Forums
The great place to discuss topics with other users
- Domicile
- Academics
- MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDAHILI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KWA KOZI ZA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 - AWAMU YA PILI
MATOKEO YA UCHAGUZI WA UDAHILI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KWA KOZI ZA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026 - AWAMU YA PILI
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 yanatangazwa rasmi leo tarehe 1 Septemba, 2025. Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi awamu ya pili katika kozi mbalimbali za afya na sayansi shirikishi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Jumla ya waombaji 15,526 waliwasilisha maombi yao kupitia CAS. Jumla ya waombaji 15,526 walikamilisha maombi yao kwa kuchagua vyuo/programu walizozipenda. Jumla ya waombaji 12,988 walikuwa na sifa kwenye programu walizoomba na jumla ya waombaji 2,538 hawakuwa na sifa kwenye programu walizoomba. Jumla ya waombaji 10,476 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi ambapo wanawake ni 5,186 (49.5%) na wanaume 5,290 (50.5%). Waombaji 330 walichaguliwa kwenye vyuo vya serikali na waombaji 10,146 katika vyuo visivyo vya serikali. Aidha, waombaji waliokuwa na sifa lakini hawakuchaguliwa kutokana na ushindani katika programu na vyuo walivyoomba, wanashauriwa kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vyenye nafasi kupitia dirisha la awamu ya tatu kwa kutumia Mfumo wa Udahili wa Pamoja. Waombaji wote wanashauriwa kuangalia matokeo ya uchaguzi wa udahili kupitia tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kwa kubonyeza CAS Selection 2025 ili kupata taarifa zaidi. Baraza linautaarifu umma kuwa dirisha la awamu ya tatu la udahili litafunguliwa rasmi kuanzia tarehe 2 hadi 26 Septemba, 2025 na matokeo ya uchaguzi wa udahili yatatangazwa tarehe 5 Oktoba, 2025 Aidha, wale wanaohitaji kubadilisha programu au chuo, dirisha la uhamisho litakuwa wazi kuanzia tarehe 2 hadi 26 Septemba, 2025, hivyo watumie dirisha hili kukamilisha maombi hayo kupitia tovuti ya Baraza kwa kubonyeza kwenye akaunti yake aliyotumia kuomba na kuchaguliwa. IMETOLEWA NA: OFISI YA KATIBU MTENDAJI BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET) 01/09/2025